Futa Akaunti Yako
Imesasishwa: 07 Agosti 2026
WingaPrime ni huduma ya JayAgric Company Limited. Ukurasa huu unaeleza jinsi ya kuomba kufuta akaunti yako na taarifa zako, na ni taarifa gani tunazolazimika kuhifadhi kwa mujibu wa sheria.
1. Jinsi ya kuomba
- Barua pepe: support@wingaprime.co.tz — andika “Futa akaunti” pamoja na jina la duka lako.
- Ndani ya app: Duka Langu → Zaidi → Futa akaunti yangu
- Kwenye Studio: Mipangilio → Futa akaunti
Tutathibitisha kwamba wewe ndiye mmiliki wa akaunti kabla ya kufuta, ili mtu mwingine asiweze kufuta duka lako.
2. Taarifa zitakazofutwa
- Akaunti yako na taarifa za kuingia
- Duka lako, bidhaa zako na picha ulizoweka
- Jina lako, namba ya simu na barua pepe
- Nyaraka za uhakiki (KYC) ulizowasilisha
- Mapendeleo yako ndani ya app
3. Kama wewe ni mnunuzi
Huhitaji akaunti kununua kwenye WingaPrime. Kama uliwahi kuomba ankara na ukatoa jina, namba ya simu au barua pepe yako, unaweza kuandika support@wingaprime.co.tz kuomba taarifa hizo ziondolewe.
4. Taarifa tunazolazimika kuhifadhi
Kumbukumbu za mauzo — ankara na risiti zilizokwisha kutolewa — hazifutwi mara moja. Sheria ya kodi ya Tanzania inatutaka kuhifadhi kumbukumbu za miamala kwa muda unaotakiwa na sheria. Kumbukumbu hizi:
- Huhifadhiwa kwa usalama na hazionekani tena sokoni baada ya akaunti kufutwa
- Hazitumiwi kwa matangazo wala hazitolewi kwa wengine
- Hufutwa kabisa muda huo unapokwisha
5. Muda
Tunashughulikia maombi ndani ya siku 30. Utapata uthibitisho kwa barua pepe akaunti yako inapofutwa.
6. Mawasiliano
JayAgric Company Limited, Arusha, Tanzania
Barua pepe: support@wingaprime.co.tz
Soma pia: Sera ya Faragha · Vigezo na Masharti
Winga